05 February 2016

Breaking News: Uamuzi wa Rais Magufuli kuhusu Air Tanzania huu hapa


combine_images

Sehemu ya hotuba ya Rais wakati akifungua mwaka mpya wa mahakama jana Februari 4, 2016.
“Kuna kesi 442 za watu waliokwepa kulipa kodi serikalini. Zile kesi kama zingeamuliwa, gharama yake ni trilioni 1. Kesi hizi zimekaa tangu mwaka 2010 mpaka leo ni 2015 …. Kwa hiyo serikali sasa hivi tumeikosa hiyo trilioni 1. Kwa trilioni 1, hata kama ungeamua Tanzania tuwe na Shirika la Ndege letu linalojitegemea, ukienda leo mka-google, thamani ya Airbus moja, mpya, brand new yenye kubeba watu kati ya 120 na zaidi ni dola milioni 90.6, ukizidisha kwa exchange rate ya sasa hivi maana yake ni bilioni 140, kwa hiyo trilioni 1 unaweza ukajua tungekuwa na Airbus ngapi mpya tumezishusha hapa. Maana yake tungekuwa na ndege zaidi ya 6 mpya, na hizi ndege tungeamua sasa badala ya kuwa msafiri anayekuja kutalii Tanzania lazima ateremkie Kenya … angeteremkia moja kwa moja Kilimanjaro na tungepata utalii …. wangekuja moja kwa moja maana yake uchumi wetu ungepanda … Nazungumza dhati kabisa na kwa uchungu mkubwa, mahakama pia mtusaidie … Ukimshika mtu red-handed, mpeleke huko huko siku hiyo hiyo akafungwe. Unahitaji upelelezi gani, umemshika na meno ya tembo, anayo mkononi, umemshika red-handed bado unazungumza kupeleleza, unapeleleza nini au unatafuta rushwa? …. Nikuombe leo Jaji Mkuu katoe hukumu ya hizo kesi 442, robo ya fedha hizo nitazileta mahakamani. Katika trilioni 1 hiyo, bilioni 250 nitazileta mahakamani ili kusudi tubaki na bilioni 750, tukanunue ndege za serikali, kwa ajili ya kuwa tuwe na Air Tanzania yenye uhakika, lakini wale wafanyakazi wa Air Tanzania, wote 200 tuwa- retrench waondoke moja kwa moja. Nazungumza hivi kwa sababu nataka mabadiliko. Haiwezekani nchi kama Tanzania, ina kila kitu, haiwezekani ikawa nchi masikini. We are supposed to be a donor country.” – Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifungua mwaka mpya wa mahakama, Februari 4, 2016

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname