24 October 2014

HATIMAYE MISS TZ NA.3 AFUNGUKIA USHINDI WA SITTI...SOMA ZAIDI HAPA


Miss Tanzania namba tatu, Jihan Dimachk. Yameongelewa mengi na kimsingi mpaka sasa bado ushindi wake unaonekana kuwa na makengeza. Kutokana na hali hiyo, waandishi wetu walifanya mazungumzo na baadhi ya wadau lakini kati yao alikuwa mmoja wa washiriki ambaye alichukua nafasi ya tatu, huyu ni Jihan Dimachk. 

Gumzo mtaani kwa sasa kwenye ulimwengu wa urembo ni ushindi wa mwanadada Sitti Abbas Mtevu ambaye hivi karibuni aliibuka mshindi katika Shindano la Miss Tanzania 2014. Tutakumbuka baada ya Sitti kutangazwa mshindi, maneno yalikuwa mengi, mara alipendelewa, mara alidanganya umri, wengine wakasema eti ana mtoto. 
Kwenye fainali za mashindano hayo mrembo huyu alichukua Taji la Miss Tanzania Top Model 2014 na sasa fuatilia exclusive enterview hii iliyofanyika kati yake na Ijumaa ndani ya Hoteli ya Regency iliyopo Mikocheni, Dar. 
Ijumaa: Habari yako Jihan, sisi ni waandishi kutoka Gazeti la Ijumaa.
Jihan: Okey, nashukuru kuwafahamu, karibuni. Ijumaa: Tuanze na matokeo ya kinyang’anyiro cha Miss Tanzania mwaka huu, unadhani wewe ulistahili kuchukua nafasi ya tatu na Sitti Mtemvu kuibuka kidedea?

Jihan: Siwezi kuongea sana jamani lakini kwa kifupi nilikuwa nikiamini nitashinda, niseme tu kwamba it was unfair but I can’t explain (haikuwa sawa ila siwezi kuelezea).

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname