24 October 2014

HAYA NDIO MAMBO AMBAYO DIAMOND NA WEMA SEPETU TU,NDIO WANAOWEZA KUFANYA HAPA BONGO!!



Diamond-Wema-Hong-Kong--slide-vibe-co-tz
Hivi ni vitu ambavyo inabidi tu tuwaachie Diamond na Wema waendelee
kufanya yao, wengine wabaki watazamaji tu, afterall siyo kila mtu yuko
kwenye movie yao ambayo bado inaendelea, hii ni moja ya celebrity couple

inayopendwa na watu wengi zaidi nchini Tzee na nje, ila kwa haya
wayafanyayo, hutakuja kuona couple wowote hapa tzee wakifanya haya
wanaofanya yao, labda huko nchi za wengine ila kwa hapa Bongo, ni Wema
Sepetu tu na Diamond Platnumz ndio wanayoweza.


Kudai kutengeneza movie ambayo haijatoka hadi leo”Temptation”

Kati ya vitu ambavyo si rahisi cople wengi kukuta wanafanya pamoja ni
movie, ila kwa hili la wapendanao hawa ni noma zaidi, ndio moja ya
celebrity couples ambao wamewahi kudai kucheza movie wakati walipokuwa
wameachana, ili tu wawe karibu pamoja, ikiwa inasemekanailikwenda
kufanyiwa shooting nchini China, na ikiwa nimwaka wapili huu sasa
wamesharudiana, na movie hiyo haijakamilika bado,huku ikibakia msemo tu
“Acha movie iendelee”.
Kuachana na kurudiana zaidi ya mara mbili.
Diamond-na-Wema-Sepetu-now-and-then-vibe-co-tz

Hawa ni moja ya celebririres waliowahi kutangaza kuachana mara kadhaa
na mwisho wa siku kurudiana na hadi hii leo bado wapo pamoja,imetokea
kusikia watu wegi maarufu hapa bongo wakiachana na kila mtu akishia
kushika mahesabu yake, ila kwa Diamond na Wema, ni moja ya couple
maarufu zilizowahi kuachana na kurudiana mara nyingi kuliko mtu yeyote
maarufu hapa Bongo. Unakumbuka yale ya Rihanna kushushiwa kipigo na
Chris Brown na bado akamrudia ?
Wema kumvalisha Diamond wigi na kupost picha mitadaoni.
Diamond-Platnumz-Wema-Sepetu-wigi

Kama ni vituko basi hapa huwa haviishi, saa zingine unaweza kusema ni
mapenzi kuzidi, ila kwa Diamond kuvalishwa wigi, kupigwa picha na
mpenzie(Wema) na kupost kwenye mitandao ya kijamii, Only Diamond na Wema
ndio kweli wanaweza kufanya hivi, katika miaka hata ya baadae, sidhani
kama watatokea couple maarufu wenye vituko kama hivi, ni nadra sana
ukute mtu maarufu wakiume kuvaa wigi la kike, kupiga picha na kupost
kwenye mitandao.
Kurekodi video  wakiwa kitandani na kupost kwa mashabiki kuangalia.
rp_wema-sepetu-akiwa-kitandani-na-diamond-platnumz-copyright-www-vibe-co-tz-web.jpg

Kama ni love ku-show love kwa mashabiki iko poa zaidi, kwa Diamond na
Wema ndio inasemekana kuwa hata baada ya kudai hapo awali kuwa kwa sasa
wanataka kuweka mambo yao yawe yao binafsi, ila ndio couple waliowazi
zaidi ku-show mambo yao hadharani, si couple wote hapa bongo wenye uwezo
wa kufanya hivi, zaidi ya kujipiga picha wakiwa kitandani na kupost
kwenye media. Tumezoea kuona watu wengi hasa maarufu wakifanya mambo yao
kwa siri zaidi, ila kwa couple hawa wako wazi sana wakifanya mambo yao.
credit : vibe

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname