Mkataba
wenya thamani ya dola za kimarekani milioni $700m uliosainiwa na washirika wa
ndege ya Etihad kwa ajili ya upanuzi wa shirika hilo umetambuliwa na shirika
lenye sifa duniani katika nyanja ya masuala ya kifedha na uchumi la “International
Financing Review (IFR)” na hivyo kuitunuku shirika la ndege la Etihad na tuzo
maalum.
Mkataba
huo wa miaka mitano ulitambulika kama dhamana kubwa kabisa ya mwaka
iliyosainiwa kutoka barana ulaya, mashariki ya kati na Afrika, katika hafla
iliyofanyika jijini London Januari 27
Mwezi
Septemba , shirika la ndege la ndege la Etihad lilianza safari ya maonyesho,
likiongozwa na mshauri mkuu, Goldman Sachs, katika bidi za kuongeza thamani ya
hisa za Shirika hilo, kampuni yake tanzu ya huduma za viwanja vya ndege ya
Etihad na washirika wengina wake watano wa huduma za angani – airberlin, Air
Serbia, Air Seychelles, Alitalia na Jet Airways – wote wakiwa ndani ya shirika
la ndege la Etihad.
Kupitia
michango ya washirika wa ndege ya Etihad BV, kikundi kilifanikiwa kupata dola
za kimarekani milioni 500, kiasi hicho kiliongezeka kwa kiasi cha dola za
kimarekani milioni 200 ndani ya siku chache tu kufuatia kuongezeka kwa shauku
kutoka jamii ya fedha ya kimataifa.
Ikiwa
kama mkataba wakifedha wa kipekee katika sekta ya masuala ya anga, hii ni mara
ya pili ndani ya wiki chache kwa shirika hili la ndege kutambulika na kupata
tuzo kupitia mkataba wake huo. Washirika wa ndege la Etihad walipokea tuzo ya
mkataba wa kifedha wa mwaka kutoka mashariki ya kati, katika hafla iliyofanyoka
jijini London kupitia Makala ya Global Transport Finance ya nchini UK.
James
Hogan, Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika la Ndege la Etihad, alisema:
“Uvumbuzi ndio msingi wa uendeshaji wa biashara zetu katika shirika hili. Tuzo
hii kutoka “International Financing Review” inaonyesha dhahiri ni jinsi gani
taasisi za kifedha zina uamini juu ya mafanikio yetu pamoja na mifumo yetu ya
kibiashara katika kuunganisha biashara zetu zite tulizo wekeza”
Akiongezea
Bw Hogan, alisema: “Katika sekta ya biashara yenye ushindani mkubwa, siri ni
kukuza uzalishaji pamoja na kuongeza ufanisi ili kukuza biashara. Kwa upande wa
wahirika, kila mmoja wao ni kujikuza kibiashara. Ila kwa pamoja, nguvu
inajumuishwa kwa pamoja. Mfumo huu wa uelewano ndio unatambua na kuidhinisha
nguvu ya shirika zima.
“Ningependa
kumshukuru na kumpongeza afisa wetu mkuu wa masuala ya kifedha, Bw James Rigney,
na timu yake nzima kwa juhudi zao za hali ya juu katika kuunda mfumo thabiti
uliokuwa kivuto katika masoko ya ndani na nje ya nchi. Walifanya kazi kwa bidii
sana kuleta shauku kubwa juu ya mifumo yetu ya kibiashara na tunayo furaha
kuona bidi zao zikizaa matunda na kupata tuzo hizi, hasahasa wakati huu ambapo
masoko mengi duniani yamejaa mashaka na wasiswasi juu ya kuwekeza fedha
kutokana na changamoto za kiuchumi duniani”.
Mkurugenzi
mtendaji wa Goldman Sachs, Bw. Martin Weber, alisema: “ Tunafuraha kubwa
kufanya kazi pamoja na washirika wa ndege ya Etihad katika kuwapatia dhamana
hii kubwa na tunapongeza timu iliyohusika katika ushindi wa tuzo ya IFR. Mafanikio
haya yanatokana na uongozi wa shirika la ndege la Etihad kukutana na wawekezaji
mbalimbali dunia nzima, na hivyo kufanikisha kukamilisha mkataba huu. Hii pia
ni ishara ya jinsi gani mfumo wao wa kibiashara ua nguvu ya kufurahisha masoko
hata katika kipindi hichi kigumu cha masoko ya dunia”
Safari
za kuchangia fedha zilifanyyika Abu Dhabi, Dubai na London zikiwa zinasimamiwa
na washauri wakuu Goldman Sachs, kampuni kutoka Abu Dhabi ya ADS Securities na
Anoa Capital. Fedha zilizopatikana ziligawanywa katika Nyanja saba tofauti,
ikiwa mchanganyiko wa matumizi ya mtaji na uwekezaji katika ndege, pamoja na
kujazia fedha kulingana na mahitaji ya vitengo mbalimbali vya shirika hili la
ndege ya Etihad.
International
Financing Review ndio chombo kinachoongoza duniani katika kutoa uchambuzi wa
kina juu ya masoko, ikitoa ushauri na uchambuzi wa kina juu ya uwekezaji wa
masuala ya kibenki kwa kauu wa benki duniani, pia hutoa habari juu ya masoko ya
kibiashara kupitia Makala zake za kila wiki ma ripoti zao za kila siku
mtandaoni
Uongozi
wa shirika la ndege la Etihad ulisifiwa na IFR kwa kukamilisha na kufanikisha
uchangishaji fedha, huku wakijenga uaminifu na kuungwa mkono na
wawekezaji.
Tukio
hilo kubwa kabisa katika kalenda ya wawekezaji masoko wa dunia kila mwaka,
litavutia wawekezaji wakubwa na wenye mafanikio zaidi ya 1,000 mwezi ujao
jijini London ili kusherekea tuzo za IFA za kila mwaka.
***MWISHO***
Kuhusu Shirika la Ndege la Etihad
Shirika la Ndege la Etihad lilianza
shughuli zake mnamo mwaka 2003 na hadi kufikia mwaka 2014, ilikuwa limeshabeba
abiria takriban milioni 14.8. Kutoka makao makuu yake huko Abu Dhabi, shirika
hili linasafiri au limetangaza mipango ya kuhudumia wasafiri na mizigo kutoka
vituo 116 huko Mahariki ya kati, Afrika, Ulaya, Asia, Australia na nchi za
Americas. Shirika lina ndege aina ya Airbus na Boeing takriban 120, Zaidi ya
ndege 200 zikiwa zimewekea oda, zikiwemo Boeing 787s 66, Boeing 777Xs 25,
Airbus A350s 62 na Airbus A380s tano.
Shirika la Etihad pia limewekeza katkia
AirBerlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Jet Airways , Virgin
Australia, pamoja na shirika lenye makazi Uswiss Darwin Airline, likifanya
biashara kama Etihad Regional. Shirika la Ethihad, sambamba na airberlin,
Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Etihad Regional, Jet Airways na NIKI, pia
hushiriki pamoja nkwatika washirika wa Etihad Airways, brand mpya inayowaleta
kwa pamoja mashirika mengine ya ndege yenye uelewa sawa ili kutoa huduma bora
zaidi kwa wateja, kuwapa wateja ratiba nzuri Zaidi na kuwazawadia wateja
wakudumu.kwa maelezo Zaidi, tafadhali tembelea :www.etihad.com
No comments:
Post a Comment