20 September 2014

KAJALA AKWAMA PESA YA KUMTOA JELA MUMEWE

Msanii wa filamu Bongo, Kajala Masanja akiwa na mumewe mahakamani.
Licha ya mkwanja kumtembelea, msanii wa filamu Bongo, Kajala Masanja amekwama kupata pesa ya kumlipia faini mumewe Faraji Chambo ili aweze kutoka jela.Akizungumzia ombi la mumewe huyo kumtaka kutofuja pesa badala yake amlipie faini ili aondokane na mateso ya gerezani, Kajala alisema ni kweli anampenda sana mumewe na angetamani kufanya hivyo lakini kiasi cha shilingi milioni 200 kinachotakiwa si kidogo hivyo hawezi kukipata.
“Nampenda sana mume wangu, hilo halina ubishi na pia najua anateseka sana kule gerezani kwani nakujua lakini milioni 200 siyo hela ndogo ujue. “Natamani hata leo niwe nayo nimlipie lakini ndiyo hivyo tena,” alisema Kajala kwa masikitiko.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname