15 April 2015

IRINE UWOYA AWEKA WAZI KILICHOMFANYA ASHINDWE KUWA RUBANI..KUMBE NI HIKI HAPA


Mwigizaji katika tasnia ya filamu Tanzania Irene Uwoya amesema kuwa filamu zimeharibu mipango yake ya miaka mingi ya kutaka kuwa mwongozaji wa ndege yaani Rubani
Irene alisema hayo weekend hii kupitia kituo cha Radio cha East Africa Radio na kudai kuwa miaka yote aliyokuwa akisoma lengo lake kubwa lilikuwa ni kuja kuwa muongozaji wa ndege Rubani kwani ndiyo kazi aliyokuwa akiipenda na alianza kusoma masomo ambayo aliamini moja kwa moja yangeweza kumfanya kufikia ndoto hizo.
Amesema ndoto yake hiyo iliingia ukakasi baada ya kuanza kufanya filamu za bongo na kujikuta sasa maisha yake yapo kwenye filamu zaidi

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname