Ujumbe wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa) upo nchini kuchunguza tuhuma za upangaji matokeo.
Waamuzi
waliosimamishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja
na watu wengine watahojiwa na ujumbe huo. Matokeo ya uchunguzi huo
yatatangazwa na Fifa baada ya shughuli hiyo kukamilika.
Tunaendelea
kuwahimiza wanafamilia wa mpira wa miguu wazidi kuzingatia kanuni za
maadili za TFF, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf) na Fifa katika
utendaji wao. FIFA itahakikisha kuwa haki inatendeka katika uchunguzi
ambao inaufanya.
No comments:
Post a Comment