Mastaa wengi wamekuwa wakiutumia mtandao wa Instagram kupost picha
ambazo zinaonesha maisha yao na karibia kila wanachofanya, lakini kwa
msanii wa R&B Juma Jux kuna mstari ambao ameuweka kati ya vitu
anavyoshare kwenye mtandao huo na maisha yake binafsi.
Inafahamika kuwa Jux anasoma nchini China, lakini hajawahi kupost picha
yoyote ikionesha yuko kwenye mazingira ya chuo kama ambavyo labda hupost
akiwa kwenye bata au akiwa na washkaji zake au kwenye show.
Baada ya kuulizwa kama kuna mambo mengine anayoyafanya huko tofauti na
chuo, na kama kweli anasoma ni kwanini hajawahi kushare na mashabiki
wake picha zozote za mazingira ya chuo, haya yalikuwa majibu yake.
“Nachoamini mimi hapa unajua mimi katika maisha yangu, Instagram ni
profile yangu mimi naamua nifanye nini sifanyi kwasababu ya watu, pia
najua mimi ni msanii kuna watu wananiangalia kuna vitu flani siwezi
kuvuka nikavifanya, “ Jux aliiambia 255 ya XXL ya Clouds Fm.
“Darasani sio sehemu ya kupiga picha umuoneshe mtu, kwanza darasani
kwetu hairuhusiwi kupiga picha, haiwezi kuwa mwalimu yupo anafundisha
halafu unapiga nioneshe watu, no. Nazingira yangu ya nje ya chuo ndio
nafanya vile haya ni maisha yangu ya nje ya chuo, lakini chuo nikienda
naenda kusoma siendi kupiga picha, kama mtu haniamini kwamba mimi nasoma
nafanya vitu vingine sina power zaidi ya kushawishi watu waniamini
zaidi ya msemo wangu kwamba mimi kule nasoma, siwezi kwenda darasani
nipige picha niko na madaftari no, lakini mimi nasoma niko kule
kwasababu ya masomo.”
No comments:
Post a Comment