Mama
mzazi wa mkali wa bongofleva Nay wa Mitego ameongea kwa mara ya kwanza
na na kusema ana wasiwasi na mwanae ambae hivi karibuni ametoa video
mpya aliyoifanya nchini Kenya.Amekiri
kweli kwamba siku kadhaa zilizopita ilibidi amwite na kumuweka chini
Nay wa Mitego akitaka amueleze kama ni kweli amejiunga na ‘freemason’
ambayo wengi wanaitafsiri kwamba ni dini ya kumwabudu shetani kitu
ambacho kiliwahi kukanushwa na aliyewahi kuwa mmoja wa viongozi wa
freemasons Tanzania.Mama
anasema alimketisha Nay chini baada ya video ya ‘Mr. Nay’ kutoka ambapo
baadhi ya picha sio za kawaida mfano damu pamoja na alama zilizotumika
ndani yake.
No comments:
Post a Comment