PREZZIE
wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel Mbwana ‘Chaz Baba’
anadaiwa nusura amtoe roho mkewe wa ndoa, Rehema Sospeter Marwa baada ya
kumpiga na kitu kizito kichwani mpaka kushonwa nyuzi ishirini.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini
ambacho kipo karibu na wanafamilia hao (jina limehifadhiwa), usiku wa
Alhamisi iliyopita, kikiwa maeneo ya Kinondoni jijini Dar kilishuhudia
ugomvi huo baada ya kwenda kuangalia nani anamshushia kipondo mwenzake.
Chanzo kilisema baada ya kufika, ndipo kiligundua kuwa, mwanamuziki huyo ndiye aliyekuwa akimpa kipondo mke wake.
“Dah!
Kiukweli kile si kipigo cha kumpiga mke, hasira bwana ni kitu cha ajabu
sana. Chaz anatakiwa kujiangalia sana,” kilidai chanzo hicho
No comments:
Post a Comment