Alhamisi
ya wiki hii Kampuni ya magari ya Nissan imezindua gari jipya lenye
uwezo wakipekee kabisa wa kujisafisha lenyewe na kuondoa kabisa uchafu
wa aina yoyote ile kwenye gari hilo.
Watengenezaji
hawa wa magari aina ya Nissan wamefanya majairibio kwenye gari hili kwa
kutumia rangi maalum ya magari inayojulikama kwa jina la "Ultra-Ever
Dry" ambayo ina ondoa uchafu kwenye gari na kufanya gari kujisafisha
lenyewe.
Kampuni ya nissan wametoa taarifa rasmi na kusema kuwa ....
"Kwa kujenga tabaka la kinga ya hewa
kati ya rangi na mazingira, kwa ufanisi kabisa inazuia maji na uchafu wa
barabara, kuunda na kuacha alama chafu juu ya rangi ya gari, " Nissan
walisema katika taarifa yao
Nissan wamesema kuwa Rangi hii inayo
zuia uchafu kwenye gari, kwa hivi sasa imefanyiwa majaribio kwenye gari
aina ya Nissan Note na imeonyesha mafanikio mazuri kabisa katika
mazingira yote ikiwa ni katika sehemu zenye hali ya hewa ya kawaida,
sehemu zenye barafu, pamoja na sehemu zenye maji maji.

No comments:
Post a Comment