28 April 2014

PICHA YA POLISI WA MWANAMKE ANAYEDAIWA KUIBA MTOTO


Mwanamama ambaye ni askari wa Jeshi la Polisi aliyefahamika kwa jina la Prisca Kilwai mwenye namba WP 5367 anayedaiwa kuiba mtoto wa jinsia ya kiume aliyefahamika kwa jina la Goodluck Salehe (siku 7).

SIKU chache baada ya kukamatwa kwa askari wa Jeshi la Polisi aliyefahamika kwa jina la Prisca Kilwai mwenye namba WP 5367 na picha yake kudaiwa ‘kuminyiwa’ na askari wenzake ili isionekane, hatimaye Ijumaa Wikienda limeinasa.

 Askari huyo ambaye kituo chake ni Ilala jijini Dar, alikamatwa kwa tuhuma za wizi wa mtoto jinsi ya kiume aliyefahamika kwa jina la Goodluck Salehe (siku 7) aliyeibwa April 6, mwaka huu huko Kasumulu Kata ya Itope Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya.


 Ilielezwa kuwa, mtuhumiwa alishirikiana na baba mzazi aliyefahamika kwa jina la Salehe Issah Mwangosi(31) mkazi wa Matankini Kyela aliyemtambulisha kwa mama mzazi (Mboka Mwakikagile umri miaka 20) kuwa Prisca ni shangazi yake hivyo amekwenda kumwona mtoto aliyezaliwa ndipo akatoroka naye.BOFYA KUSOMA ZAIDI

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname