11 April 2015

DIAMOND PLATINUMZ ANENA MAZITO KUHUSU WEMA, AJIAPIZA KIFO! WEMA NAYE AJIBU MAPIGO!


Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’.
Musa mateja KIAPO! Kuonesha kwamba hana mpango wa kurudi nyuma, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ amefungukia msimamo wake juu ya mwandani wake wa zamani, Wema Sepetu ‘Madam’ kwa kusema kuwa kamwe hawezi kumrudia tena, Risasi Jumamosi lina mkanda kamili.
Licha ya Diamond kufunguka hayo, wawili hao wamekuwa na mapenzi ya vipindi, kuna wakati waliwahi kumwagana kisha kurudiana na hakuna aliyewahi kutoa tamko zito lakini safari hii Diamond amesema ndiyo basi tena!

TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na staa huyo, mara kwa mara Diamond amekuwa akijiwekea nadhiri ndani ya moyo wake na kusisitiza kwamba pamoja na kuwa maisha ya sasa huendeshwa kwa msingi wa fedha lakini hata kama ‘atafulia’ kiasi gani, ni bora afe maskini kuliko kurudiana na Wema.
“Diamond amekuwa akisema kila wakati kwa msisitizo kuwa kutokana na matatizo aliyokumbana nayo katika uhusiano wake kwa Wema, ni vigumu sana kurudiana naye wala kuwaza kama ipo siku anaweza kuwa naye, maana hakuna tena jambo geni asilolijua kwake,” kilisema chanzo hicho na kufunguka zaidi:SOMA ZAIDI>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname