28 April 2014

DIAMOND ANATAFUTWA CHINA.....ALIYEJIFANYA DANSA WAKE ADAKWA NA MADAWA YA KULEVYA


STAA  wa  muziki  wa  bongo  fleva  nchini, Abdul  Nassib  "Diamond"  ametakiwa  kutokanyaga  kabisa  nchini  China  na  kwamba  akitokeza  pua  yake  nchini  humo  asahau  kabisa  kurudi  uraiani... 
Hiyo  inafuatia  kijana  mmoja  mtanzania  kukamatwa  wiki  iliyopita  uwanja  wa  ndege  wa   Macau   China  na  kudai  kuwa  yeye  ni  mcheza  shoo  wa  mwanamuziki  Diamond  kutoka  Tanzania....
Habari  kutoka  Macau  China  zinadai  kuwa  kijana  huyo  aliyejulikana  kwa  jina  moja  la  Manyota  alikamatwa  akiwa  kwenye  harakati  za  kuingiza   mzigo  huo  wa  dawa  za  kulevya  kwa  kupitia  uwanja  wa  ndege  wa  Macau....
Kwa  mujibu  wa  vyanzo  vyetu  vya  habari, inaarifiwa  kuwa  Manyota  alikamatwa  Alhamisi  ya  wiki  iliyopita  katika  uwanja  uleule  aliokamatwa  mtanzania  mwingine  Jackline  Patrick, anayesotea  rumande  mpaka  hii  leo  huko  huko  Macau  China.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname