Breaking Newss Taarifa zilizotufikia hivi punde kutoka chanzo chetu cha habari kinasema boti ya MV Kilimanjaro II mali ya Bharlesa imepigwa na dhoruba maeneo ya kisiwa cha Nungwi imekosakosa kuzama ikiwa inatoka Pemba kuelekea Unguja kwa mujibu wa mtoa habari wetu ni kwamba kuna Abiria wengine wameachwa baharini pamoja na mizigo mingine kutokana na Boti hiyo kupigwa na wimbi kubwa na kuyumba na kujikuta kuwadondosha abiria pamoja na mizigo katika bahari kwa sasa boti hiyo inaendelea na safari,
mabaharia wa Boti hiyo wamejitahidi wamewarushia maboya abiria hao ambao inasadikiwa ni zaidi ya kumi ambao wamewaacha eneo hilo chafu karibu na kisiwa cha Nungwi eneo ambalo ni chafu sana kwa vipindi mbali mbali katika bahari ya Hindi, tatizo la ajali hiyo inasadikiwa ni kutokana na upepo mkubwa uliotokea maeneo hayo na si Boti hiyo kujaza abiria kwa mujibu wa mtoa habari wetu.INAENDELEA

No comments:
Post a Comment