Taarifa
za msanii Mez B kushambuliwa na mtu asiemfahamu wala kuwa na ugomvi nae
usiku wa Jumamosi akiwa maeneo ya Sinza ni miongoni mwa stori
zilizosambaa sana toka jana.
Mez B kwenye interview fupi na millardayo.com amesema amepata
majeraha mengi maeneo ya usoni na anasema kwamba kuna kisu alikikwepa
kikielekezwa shingoni wakati aliporushiwa visu mbele ya Mabaunsa wa
sehemu ya burudani Sinza waliokua wakishuhudia bila kutoa msaada wowote.
Mez B tayari ameshaifikisha hii ishu kwenye vyombo vya sheria ili
kila kitu kikae kwenye mstari kuhusu mtu huyu aliemshambulia ambae Mez
anadai alimkuta mahali anasubiria kufungiwa chips zake ndio akaanza
kutukana watu mbalimbali ikiwemo Serikali na Mez B mwenyewe.
Baada ya hapo wakati Mezi akiondoka, baunsa mmoja kwenye eneo hilo
alimwita na kumwambia haiwezekani huyu jamaa akutukane hivihivi hebu
njoo tumuulize, tofauti na alivyotarajia…
Mez anasema yule Baunsa ndio
alimfata yule mchoma visu na kumwambia amalize kazi, yani akamshambulie
Mez B.
No comments:
Post a Comment