05 January 2014

WIVU WA MAPENZI ULIVYOUA WENGI 2013

 Christina Alfred akiwa amejipumzisha nyumbani kwao Ilala baada ya kutoka hospitali kutibiwa jeraha la risasi. Picha ya Maktaba  

Tumefunga mwaka 2013, milio mingi ya risasi ilisikika, watu walipigwa mapanga,  wengine kunywa sumu kutokana na kukithiri kwa matukio mbalimbali yanayoambatana na visa na visasi vya wivu wa mapenzi yaliyojeruhi hata kupoteza maisha ya watu.
Matukio ya wivu wa mapenzi yalikithiri miongoni mwa jamii katika mwaka uliopita, hali iliyojenga hofu na kuondoa furaha ya kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi.
Wachambuzi wa masuala ya uhusiano wanasema kuwa hatua hiyo inatokana na idadi kubwa ya wapenzi kukosa uaminifu, kutokana na tamaa ya fedha, udhaifu wa kingono, tendo la ndoa, kasumba, tamaa za kimwili na mambo kama hayo. Baadhi ya takwimu za matukio hayo zinaonyesha kuwa kwa Mkoa wa Tanga pekee kuanzia Januari hadi Agosti mwaka jana, watu 16 waliuawa katika matukio 377 ya wivu wa mapenzi, baada ya kukamatwa ugoni.
Mbali na takwimu hizo, ipo baadhi ya mifano iliyojitokeza katika kipindi cha kuanzia Januari mpaka Novemba 2013 hapa nchini.
Baadhi ya matukio yaliyojitokeza mwaka 2013
Novemba 13, mwaka huu, Mzee Juma Kondo (80), Mkazi wa Mkuranga mkoani Pwani alijiua kwa kunywa dawa ya macho kutokana na wivu wa kimapenzi.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana katika eneo la tukio. Mzee Juma alikuwa akimtuhumu mkewe Asha Ali (50), kutembea na mtoto wao wa mwisho aliyekuwa na umri wa miaka 12, madai yaliyoelezwa kuwa ni ya muda mrefu.
Mke wa marehemu(Asha), alikiri mumewe kujiua kutokana na wivu huo wa mapenzi.SOMA ZAIDI

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname