Habari zilizopatikana kutoka katika eneo la tukio, zinasema mchungaji huyo, Owiti Ariri aliuawa muda mfupi baada ya kukabidhiwa sanduku la fedha za kikundi chao cha kuweka na kukopa alichokuwa akikifanyia kama mweka hazina.
Habari zilizothibitishwa na mchungaji mwenzake,
Christopher Nyaitega, zinasema tukio hilo lilitokea juzi katika moja ya
hoteli iliyoko katika mji huo.Mchungaji Nyaitega ambaye hata
hivyo hakuweza kujua kiasi cha fedha kilichokuwemo ndani ya sanduku hilo
kwa kuwa yeye siyo mmoja wa wanakikundi, alisema wanakikundi waliamua
kumkabidhi fedha hizo ili azipeleke benki kesho yake.
Alisema akiwa nyumbani kwake, alifikiwa na mmoja
wa wanakikundi wenzake aliyeanza kudadisi kuhusu fedha hizo, ambapo marehemu alimhakikishia kuwa ziko salama hali iliyomfanya mgeni wake huyo aondoke.
Alisema muda mfupi baada ya mgeni huyo kuondoka, ghafla majambazi walifika nyumbani hapo na kumtaka marehemu awape fedha hizo kabla ya kumuua.
Alisema jeshi hilo linamshikilia mwanakikundi huyo kwa mahojiano zaidi, huku akiahidi kutoa taarifa zaidi kuhusiana na tukio hilo leo.

No comments:
Post a Comment