22 December 2013

BOB JUNIOR"NDIO NI NGUMU SIKUWA NA FURAHI...SITAOA TENA..UBACHELOR RAHA


Rais wa Masharobaro, Bob Junior amesema hakuwa na furaha kwenye ndoa yake na ndio maana ameachana na mke wake.

Muimbaji na mtayarishaji huyo wa muziki aliiambia tovuti ya Times FM kuwa ugumu wa ndoa umemfanya asifikirie tena kuoa maishani.

“I’m single, sitaoa tena…mimi niko single na sitaoa tena. Kwa sababu nimeona ugumu wa ndoa na wepesi wa kuwa bachelor. Kwa hiyo nimeamua kuwa bachelor na siwezi kuoa tena, sioi tena jamani I’m single. No more kuoa Bob Junior,” aliiambia tovuti huyo.

“Unajua unapokuwa kwenye mahusiano ya boyfriend na girlfriend, hamna ile ‘uko wapi sasa hivi, rudi haraka nyumbani’, umeenda kwenye show ukirudi mara kanuna.”

Bob Junior aliiambia tovuti hiyo kuwa ndoa yake ilikuwa ikirudisha nyuma maendeleo ya kazi yake kwa kuwa katika siku saba za wiki ni siku mbili tu anakuwa na furaha, na kwa kuwa kazi yake inategemea ubunifu na utulivu asingeweza kufanya kazi vizuri

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname