22 December 2013

INSTAGRAM NI MTANDAO UNAOONESHA MAISHA YA UONGO NA KWELI

Ukiwa na roho nyepesi na mtu unayeumizwa roho kirahisi na maisha mazuri ya watu wengine, Instagram sio mtandao unaokufaa. Hata hivyo, usiamini kila picha unayoiona kwenye Instagram. Hii ni kwasababu watu wengi wamekuwa wakiitumia kuishi maisha fake na kuigiza ambayo hayana hata asilimi 10 ya uhalisia. Unaweza ukaingizwa mkenge na picha zinazooneshwa watu wakiishi maisha ya kifahari kumbe maisha yao halisi niya kustaajabisha.

Ipo mifano mingi ya watu wanaoweka nyumba ama magari ya kufahari na kusema ni yao wakati sio kweli. Instagram haiwezi kuonesha maisha halisi ya watu japo baadhi ya wale wanaoonesha maisha ya kifahari kwa picha zao wanayaishi kweli.


 Ni sehemu ya kuonesha chakula kitamu ulichoagiza kwenye hoteli za bei za juu na kuwaumiza roho wengi. 

Mtandao huo wa kijamii umejipatia sifa ya kuonekana kuwa mtandao wa kishua kuliko mingine yeyote. Hii ni kwasababu application yake inapatikana kwenye smartphones peke yake, tofauti na mingine kama Facebook ambayo Irene Uwoya anaichukulia kama ‘daladala’. Instagram imechuja watu na kwa Tanzania imeonekana kupendwa.


Hiyo ndio sehemu iliyotawaliwa na selfie – picha za kujipiga mwenyewe, kawaida ama kusimama kwenye kioo.


Ni sehemu ambayo wasichana waliojaaliwa neema za Mungu huko nyuma kama akina Agnes Masogange, huitumia kunadi asset zao.


Instagram ni sehemu ya kuonesha mijengo inayojengwa na wasanii na watu wengine waliojaaliwa kipato.


Ni sehemu ya kwanza kuiweka picha ya gari lako lako jipya ulilolinunua ili kuwaonesha watu kuwa wewe si size yao, wewe ni matawi mengine kabisa.



Watajuaje kuwa biashara ama mchongo unaofanywa umefanikiwa kama usipoweka picha za noti nyingi za dola kama Irene Uwoya anavyoumiza roho za kwanini:

“Haya wenye kuniagiza ndooomda huuu….minimemaliza kila kitu…afu bado pesa nyingi zabak….inabidi ziiiiiiiishe….niagizen bwanaaaaa…….kama nawaona wenye roho za kwanin…sio mim ni MUNGU,” ameandika Irene kwenye picha ya chini aliyoiweka Instagram.


Ama Diamond alivyoandika kwenye picha yake: Rubber band for what…???? Money is tied by Money #USD #Gold #Valuables #WCB for Life mama.”


Au Jux alivyoweka picha hii:


Instagram ndio sehemu ya kuwaonesha watu nguo, viatu ama vidani aghali unavyovaa.


Kwa mifano hiyo, picha hizi za kuumiza roho wengi zimepewa jina ‘braggie’ ikiwa na maana ya picha inayowekwa kwenye mitandao ya kijamii kushow off ama kuwatia wivu washkaji, na kwa mujibu wa utafiti, mmoja kati ya watuamiji 10 hufanya hivyo mara kwa mara.
Picha kama watu wakiwa kwenye vyumba vya hoteli, bar ama kwenye nightclubs si ngeni kwenye macho yako kama upo Instagram

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname