Mastaa wa filamu za Kibongo wenye jina kubwa mjini, Aunt Ezekiel, Jacgueline Wolper
na Snura Mushi hivi karibuni walitisha kwa kufunga mtaa kutokana na mauno
waliyokuwa wakikata mbele za wapiga ngoma wa Kundi la Baikoko, tukio lililojiri
Mwananyamala, Dar nyumbani kwa msanii mwenzao Vanitha Omary...Endelea hapa chini..
Wasanii hao
waliwashangaza watu jinsi walivyokuwa wakijituma kukata mauno huku Wolper
akimtunza mpiga ngoma na kumkatikia kwa staili mbalimbali zikiwemo za chumbani.
“Yaani wewe
ulikosa mambo, Snura alitoa shoo na mapacha wake utadhani alikuwa
amelipwa, yaani walinogesha ngoma ya kumuaga mdogo wake Vanitha ambaye
anakwenda kufunga ndoa Dodoma,” alisema sosi aliyekuwa akimsimulia mwandishi
wetu.
Aidha, wageni
waliokuwa wamealikwa eneo hilo hawakudhani kama Wolper na Aunt wangeweza
kujituma vile kama walivyokuwa wakikata mauno hayo kwa sababu ustaa wote
waliuweka pembeni na kujiachia kwa raha zao.
source:Globalpublishers
No comments:
Post a Comment