STAA wa Bongo Fleva,Naseeb Abdul’Diamond amefunguka kuwa yuko tayari kwenda jela kama atatokea mtu yoyote akamchezea au kumdhalilisha kwa namna yoyote mama yake mzazi Bi.Sanura Kassim.
Akizungumza
kupitia kipindi cha Take One cha Clauds TV na Zamaradi Mketema hivi
karibuni alisema kuwa ni bora hao watu wakamchezea yeye(Diamond) hasa
waandishi wanavyomdhalilisha kwenye magazeti kwa kuandika habari za
uongo juu yake kuliko kumuandika na kumdhalilisha mama yake kwa habari
za uongo.
‘Niko
radhi kwenda jela kama itatokea kwa mtu yoyote yule akimdhalilisha mama
yangu kwani nitamfanya kitu kibaya ambacho kitanifanya nishtakiwe na
nipelekwe jela ni bora unichezee mimi kuliko mama yangu ni kila kitu
kwangu sipendi mama yangu apate shida,alisema Diamond.
Pia
alipoulizwa katika maisha yake aliwahi kwenda kwa mganga alisema kuwa
hajawahi na kwamba haamini ushirikina na anamwamini Mwenyezi Mungu.
No comments:
Post a Comment