09 October 2013

MSANII NONINI WA KENYA AFUNGUKA KUHUSU SHUTUMA ZA KUA KATIMULIWA KAZINI


Nonini kipindi hicho akitangaza kipindi cha asubuhi OneFm huko Kenya.
Msanii Nonini Mgenge kutoka Kenya ambaye pia alikuwa mtangazaji wa OneFm amesema kuwa ameacha kazi hiyo ya utangaji kutokana na sababu zake bonafsi ambazo hayuko tayari kuziongelea.Nonini alisema pamoja na hayo utangazaji ni kazi anayoipenda na hawezi kuiacha kabsaa hivyo ataendelea kuifanya.
Msanii huyo alisema kuwa wakati anafanya kazi hiyo alikuwa anapata wakati mgumu kupiga nyimbo zake lakini ilimbidi wakati mwingine apige pale unapokuta wasikilizaji wengi wameuomba.Msanii huyo ambaye aliwahi kutajwa na mtandao mmoja kama msanii wa muziki mwenye like nyingi zaidi kuliko wasanii wote Africa ya Mashariki alisema pamoja na ushawishi wake kwenye mitandao yake,na brandy ya jina lake hana mpango wowote wa kuja kuingia kwenye siasa.

SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname