KATIKA hali isiyotarajiwa katika wasanii wanaounda kundi la Bongo
movie wamejikuta wakijitenga kushiriki msiba wa Baba mzazi wa msanii
mwenzao Wema Isack Sepetu, baada ya kuundwa zengwe na mmoja wa watu
wenye ushawishi katika kundi hilo, Wema akiongea kwa uzuni amesema kuwa
hata wale waliofika jana katika msiba huo hawakufika kwa ajili ya
kumfariji bali walifika kwa ajili ya kumsanifu.
FC ilifanya utafiti ili kubaini hilo kwa kuwapigia simu baadhi ya
wasanii wanaotoka katika kundi hilo nao bila kusita kwa masharti ya
kutotajwa majina walitiririka kwa kusema kuwa ni kweli uongozi wa kundi
hilo umetoa agizo watu wasishiriki kutokana na tabia ya msanii huyo
kutoshiriki katika misiba ya wasanii wenzake.
“Ni kweli hilo lipo na lina ukweli kwa njia moja au nyingine Wema
bwana huwa hashiriki katika misiba ya wasanii wenzake, kuna mtu muhimu
sana na ana sauti katika kundi la Bongo Movie amesema kuwa katika misiba
iliyotokea ameshiriki misiba miwili tu, wa marehemu Sharo na Kanumba
kwa sababu alikuwa mtu wake,”anasema kijana huyo.
Hili si jambo la kulifurahia kwa wasanii kwani halijengi bali
linaleta mgawanyiko wa moja kwa moja, msanii mwingine alikiri kuwa Wema
anabagua kushiriki misiba kwani wakati amefariki marehemu John Maganga
alipigiwa simu ili ashiriki katika msiba lakini alisema yupo Location,
hivyo wasanii wenzake wanamtenga ili aone umuhimu wa kushiriki misiba ya
wenzake.
Jana jioni nyumbani hakukuwa na wasanii zaidi ya mtangazaji wa
kipindi cha Take One Zamaradi Mketema akiwa na Rais wa shirikisho la
wasanii Simon Mwakifwamba na waombolezaji wengine, huku baadhi ya
wasanii wakifika pale na kuondoka jambo ambalo Wema alilitafsiri kama
walifika pale kutoa lawama ili asiwaone kama hawajafika lakini hawakuwa
na dhamira ya kweli mioyoni mwao.
No comments:
Post a Comment