09 October 2013

Basata yatoa Kalipio kali kwa Mratibu wa shindano la Miss Utalii

Miss utalii Tanzania 2013, Hadija Mswaga (kushoto) akiingia kwenye Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana, kuelekea Equatorial Guinea kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Dunia ya Miss Tourisim World 2013, pembeni ni mshindi wa tatu, Teresia Kimolo. aliyemsindikiza (Picha na Hosea Joseph)

BARAZA la Sanaa la Taifa (Basata), limempa karipio kali Mwenyekiti wa shindano la Miss Utalii, Gideon Chipungahelo kwa kosa la kudhalilisha baadhi ya washiriki na malalamiko kufanyiwa kazi na Baraza hilo.

Karipio hilo lilitolewa baada ya Basata kupitia tathmini iliyohusisha vipande vya matukio yaliyorekodiwa (clips) na kujionea namna wasichana wanavyofanyiwa vitendo vya udhalilishaji na Chipungahelo kwa kipindi cha  kambi ya miezi mitatu.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname