04 February 2016

SIMBA HADI RAHA SPIDI 120Tangu aanze kuingoza Simba, kocha Jackson Mayanja amekuwa akipata matokeo chanya huku leo wakipata ushindi mnono wa mabao 5-1 dhidi ya Mgambo JKT  mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Hamis Kiiza aliipatia Simba bao la mapema dakika ya tano kabla hajakosa penati iliyotokana na beki wa Mgambo kuunawa mpira katika harakati za kuokoa. Kiiza alipiga penalt dhaifu iliyoishia mikononi mwa kipa Mudathir Hamis.
Dakika ya 29 Mwinyi Kazimoto aliipatia Simba bao la pili kwa shuti kali la nje ya 18 baada ya kutokea piga nikupige. Simba iliyotawala mchezo huko kwa kiasi kikubwa ilipata bao lake la tatu katika dakika ya 42 kupitia kwa Ibrahim Ajib akimalizia pasi ya Jonas Mkude.
Danny Lyanga aliyeingia kuchukua nafasi ya Ajib aliipatia Simba bao la nne dakika 77 kabla Kiiza hajafunga kitabu cha mabao ya leo kwa bao la dakika ya 82.
Ikionekana kama vile pambano hilo lingeisha kwa matokeo ya 5-0, Fully Maganga alichafua rekodi safi ya Mayanja ‘Clean Sheet’ kwa kuipatia Mgambo bao la kufutia machozi  dakika ya 88.
Katika mchezo huo Mayanja aliwapumzisha Hija Ugando na Justice Majabvi na kuwaingiza Brian Majwega na Said Ndemla. Kocha wa Mgambo, Bakar Shime aliwatoa Bakari Mtama na Ramadhan Malima huku akiwaingiza Boli Shaibu na Mussa Ngunda.
Kwa matokeo hayo Simba imefikisha pointi 39 sawa na Yanga pamoja na Azam lakini bado wapo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname