04 February 2016

YANGA HALI BADO TETE YAPONEA CHUPUCHUPU MBEYAMabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga leo wamelazimisha sare ya bao 2-2 dhidi ya Prisons katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Matokeo hayo si mazuri kwa Yanga kwani wanaendelea kujiweka katika mazingira magumu ya kutetea ubingwa woa japokuwa bado wapo kileleni kwa pointi zao 39 sawa na Azam pamoja na Simba ingawa wanatofautiana kwa mabao ya kufunga.
Yanga ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia straika wake Amissi Tambwe aliyefunga kwa kichwa dakika ya 36  na baadaye Jeremiah Juma alisawazisha bao hilo dakika ya 41. Matokeo hayo yalikwenda mpaka wakati wa mapumziko.
Dakika ya 63, Prisons iliongeza bao la pili mfungaji akiwa ni Mohamed Mkopi akimalizia mpira wa faulo uliopigwa na Meshack Seleman huku Yanga wao wakisawazisha dakika ya 85 kwa mkwaju wa penalti iliyopigwa na Simon Msuva.
Mtibwa Sugar wao wamelala nyumba kwa mabao 2-0 dhidi ya Toto Africans ya jijini Mwanza mabao yote yalifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Simba, Christopher Edward wakati Kagera Sugar nao wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Majimaji, mechi iliyochezwa Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname