04 February 2016

Nay Wa Mitego kupelekwa mahakamani kisa haya mashairi yake nayayo waponda tasnia ya Bongo Movie!

Nay%2Bwa%2BMitego
Rapa Nay Wa Mitego baada ya hivi karibuni kupost katika mitandao ya kijamii mashairi ya wimbo wake mpya yenye ‘utata’, mmoja kati ya wasanii wa Bongo Movie Kajala Masanja ametishia kumpeleka mahakamani.

Kupitia instagram, Nay wa Mitego aliandika "Mungu akunyimi vyote lazima atakupa chako, Demu anasura mbayaa lakini ana Bonge la Tako. BongoMovie Imekufa wamebaki kuuza Sura, Wote wanataka Kuimba Kama Shilole Snura. Ray Kigo kawa Mkongo Mpaka Leo anaishi kwao, hela za kuuza Movie zote ananunua Mkorogo... Kuna Nivar super Marioo ana Gari la Milioni Kumi ajawai ata miliki Getto, anaishi kwa Mademu wakiachana Gari ndio Geto. Kuna Wasanii Mapunga walio ponzwa na tamaa..."
Kajala%2BMasanja

Baada ya kauli hiyo, mwanadada wa filamu Kajala Masanja aliimbia Clouds Fm kuwa hawafurahishwi na kauli za Nay.

“Nyie mnacheka mnaona sifa huyo anatukana. Wakati sisi Bongo Movie wote tuna uwezo wa kumshtaki, hawezi kututukana hivyo yeye ni nani?, mnakaa mnadhalilishwa mnafurahi,’’ alisema Kajala.

Hata hivyo, Nay wa Mitego baada ya kusikia kauli ya Kajala alijibu mapigo.

“Nimesikia kuwa Bongo Movie wana mpango wa kunipeleka mahakamani, nimeongea na wakili wangu kaniambia tutashinda kesi . Halafu Kajala namuheshimu sana kama mama yangu, nimemsikia alichosema nasubiria wanipeleke mahakamani,” alisema Nay

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname