04 February 2016

INASIKITISHA SANA ....Mwanafunzi kutoka Tanzania ameshambuliwa na kuvuliwa nguo NCHINI India


Mwanafunzi mmoja kutoka Tanzania ameshambuliwa na kuvuliwa nguo na kundi la watu wenye hasira katika jiji la Kuisini mwa India la Bangalore. Tukio hilo limetokea baada ya gari lililokuwa likiendeshwa na mwanafunzi kutoka Sudan kumgonga mwanamke mmoja na kumuua. Kundi hilo la watu lilimshambulia mwanafunzi wa kike kutoka Tanzania mwenye umri wa miaka 21 akiwa pamoja na rafiki zake watatu- wote kutoka Tanzania- wakati wakipita katika eneo la tukio hilo. Kundi hilo lilimfukuza mwanafunzi huyo na kumvua blauzi yake, wamesema polisi. Taarifa zinasema ubalozi wa Tanzania nchini India unatafuta maelezo zaidi kuhusiana na tukio hilo. Tukio hilo limetokea siku ya Jumapili usiku, lakini liliripotiwa kwa mara ya kwanza siku ya Jumanne. Polisi wameiambia Idhaa ya Hindi ya BBC kuwa kundi hilo mjini Bangalore lilikusanyika katika eneo la Hessargatta baada ya mwanafunzi kutoka Sudan kumgonga mwanamke mmoja aliyekuwa amelala kando ya barabara. Kundi hilo la watu lilifanikiwa kumpiga mwanafunzi huyo na kuteketeza kwa moto gari lake, lakini alifanikiwa kukimbia.

1 comment:

Comments system

Disqus Shortname