16 January 2016

Stara Thomas: Sikuamiani Jinsi Sugu Alivyojifanya Hanijui Bungeni

STARA
Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio Ijumaa hii, Stara alisema hakutegemea kutokea kwa hali hiyo kwani yeye aliwahi kumsaidia Sugu katika kipindi cha nyuma wakati akiandaa wimbo wake Mr II.
“Sugu anakuja nyumbani mimi nanyonyesha, ‘dada dada mimi siwezi kufanya kazi peke yangu’” alisema. “Halafu nimekutana naye Dodoma ananipita kama hanijui. Kitu ambacho nakumbuka Sugu na mimi tulikuwa tunawasiliana kwenye simu akasema ‘Stara mimi nakuja na nyimbo yangu mpya.’ Lakini alikuja kipindi ambacho mimi najifungua mtoto wangu wa pili, nilikuwa na kama miezi miwili. Kwahiyo aliniomba ilikuwa ni ngumu kwa sababu nilikuwa nanyonyesha, nikasema ‘any way wewe ni wangu nikaongozana naye mpaka studio na nilikuwa narekodi huku tukipokezana mtoto,” aliongeza Stara.
Aliongeza, “Lakini kilichoniumiza kuna wakati nilikutana naye bungeni kiukweli hiki naomba nikiseme. Adabu aliyonionyesha Sugu ilikuwa sio. Kwa sababu Sugu sio wa kunipita mimi bila kunisalimia, sisemi kwa ubaya lakini kwa mtu ambaye mimi nilimpokea nikiwa na mtoto mchanga, nikaenda naye studio na mtoto mchanga kwa mapenzi yote haijalishi hata kama kuna mapungufu hata mpo katika vyama tofauti. Najua yule yupo kwenye chama kingine na mimi nipo CCM, kwahiyo alionyesha zile chuki za kisiasa.”
Credit; BongoMovie

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname