06 February 2014

Namna ya kuondoa uchawi mwilini na kufukuza majini

Maelekezo ya dawa ni bure na utaratibu utapewa na mjina ya madawa utapewa utafute madukani na utapata ili usidanganywe na kutolewa pesa nyingi kila mara na waganga wenye kufanya wanadamu wenzao wenye matatizo ya kiuchawi na ushirikina kama miradi yao ya kuchuma pesa.

Kwanza kabisa uchawi upo, hii inatokana na maandishi yaliyoko kwenye vitabu vya dini kama Qur'an, Injili, Taurati, Zaburi. Pia matukio ya kukamata wachawi usiku na wao kukiri kuwa wanaroga wenzao, kwa sasa watu wanaologwa idadi imeongezeka na uchawi umekithiri.

Ukitaka kujua zaidi fuatilia kwenye mtandao vyuo vya kufundisha uchawi vimezidi kuanzia ulaya hadi Asia ni vya wazi ila Africa bado ni vya kuficha, hii inaonyesha shetani alivyo jizatiti kinguvu za giza.

Msaada kwa mwanadamu ili aepuke janga hili ni kumtegemea Mwenyezi Mungu mmoja aliyeumba kila kitu na hata huyo sheitwani ni kiumbe chake, ukiisha mtegemea Mwenyezimungu kiukweli kwa dhati ya kutoka moyoni mwako kuwa anaweza kushinda basi atashinda kweli, na hii iambatane na kuacha maasi kama zinaa, wizi, uongo, fitina, husuda ya uadui, ushirikina, pombe, kula riba, rushwa, n.k

Jeshi la Mwenyezi Mungu muda wote ni lenye kushinda na jeshi la sheitwani yaani majini, wachawi, mizimu, n.k ni vyenye kushindwa vibaya sana.

kwa hiyo Dawa hii ya kuondoa uchawi mwilini iambatane na Imani ya kuamini Mwenyezi Mungu Mmoja na kuamini kuwa Mitume wote walikuwa wajumbe wake kwa mwanadamu ili aongoke na kuamini kuwa Mtume Muhammad (SAW) ni mtume wa mwisho na ni kwa ajili ya ulimwengu wote.Kuota ndoto za kutisha, kulishwa vitu, kuchanjwa usiku, kuota unafanya mapenzi na watu wa kutisha, wanyama, n.k

Hii hali ya Kuota ndoto za kutisha, kulishwa vitu, Kuota ndoto za kutisha, kulishwa vitu, kuchanjwa usiku, kuota unafanya mapenzi na watu wa kutisha, wanyama, n.kuchanjwa usiku, kuota unafanya mapenzi na watu wa kutisha, wanyama, n.k ni dalili za wachawi wanaotumia majini na mizimu kuingia ndani ya nyumba usiku na kuchezea wanadamu wenzao. Hii na silazilama waje usiku hata wakiwa mbali wanaweza wakatuma mashetani ambao wamefanya urafiki nao kwa kutii amri za mashetani badala ya Mwenyezi Mungu Muumba kwa kufanya makafara mara kwa mara.
Tiba ya kufukuza ndani ya nyumba zipo zaidi ya moja lakini nyepesi ni ya kujifukiza na kufukiza nyumba ndani dawa, dawa hii ni kama unavyo nunua dawa ya mbu au wadudu ukawafukuza na kuwaua kwa kupulizia ndani ya nyumba.
Kama mtu anaota ndoto za kutisha na kufanyiwa mambo mabaya usiku kama mwanamke kuingiliwa na mwanaume kuota anafanya mapenzi na mwanamke asiyemjua na hata akiwa anamjua. Asubuhi kuamka umechanjwa au una mikwaruzo mwilini usiyojua chanzo chake au kuamka umeteguka mguu au kukata tamaa na kujiona hufai, kuchukiwa na kila mtu, n.k
Tiba ya hali hii na kupata dawa ya mchanganyiko ya kujipaka mwili mzima kabla ya kulala ili masheitani na uchawi vinavyokusumbua na kukuweka katika mazingira yasiyokuwa ya kawaida kisaikologia vyote viondoke na uwe salama kwa Uwezo wake Mwenyezi mungu. Na hata mchawi akija kukugusa usiku atapata cha moto ukiwa umelala umejipaka dawa hii katika hali ya mafuta.

Kwa maelezo zaidi: tibaherbs@gmail.com: Simu:0764244867/0785883692
Dawa ya kunywa
Tafuta majani ya Sanamaki
Chemsha viganja viwili(Chota viganja viwili vya majani ya sanamaki)
Chemsha kwenye lita tatu za maji mpaka zibaki lita 2 na nusu na toa motoni poza)
Chuja na weka asali nusu lita
Kunywa asubuhi glass moja na jioni moja mpaka iishe
Utasikia tumbo limebadilika na utaharisha uchafu uliopo tumboni na baadaye utakuwa sawa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu

Dawa ya kujifukiza kila asubuhi na jioni hasa hasa kwa mtu mwenye kusumbuliwa na majini

Tafuta dawa hizi
kibiriti upele unga
Camphor(Kafuri ni kama vipande vya square na ni vyeupe kama chumvi)
Altiti(mvuje)

changanya pamoja vijiko vitatu vya mvuje(Altiti) na hizo dawa yaani kibirit upele na camphor(kafuri)

Utakuwa unajifukiza kijiko kimoja cha chai asubuhi na jioni ukiwa umejifunika shuka na uhakikishe mwili mzima unapata moshi wa dawa hasa kuanzia shingoni na kifuani

dawa ya kujipaka
Tafuta mafuta ya zaituni changanya na mvuje vijiko vya chai viwili tingisha na pia weka camphor(kafuri) kijiko kimoja tingisha upate solution iliyo na mvuje, zaituni na Camphor

hii utakuwa unajipaka mwili mzima hasa sehemu zinazoumwa na unaposikia vitu vinatembea tembea mwilini

watoto wanasutuka usingizini na kulia mara kwa mara usiku wapake dawa hii watasinzia vizuri Kwa uwezo Mwenyezi Mungu.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname