27 January 2016

KIMENUKA BUNGENI: BUNGE LAAHIRISHWA, CHANZO NI ZITTO KABWE

Bunge laahirishwa ghafla, ni baada ya Zitto kuomba Muongozo

Mwenyekiti wa Bunge Andrew Chenge, amesitisha shhughuli za bunge kwa saa moja Ni baada ya bunge kulalamikia kutooneshwa live Mikutano ya bunge.

Zitto Kabwe (mbunge) aliomba Muongoza wa kuahirisha bunge kwa sababu kwamba, hawawezi kuendelea kujadili Hotuba ya rais iliyooneshwa live wakati bunge halipo live. Wanachotaka ni Bunge kuwa live sababu, TBC1 ni mali ya Umma na haijiendeshi kibiashara.

Hivyo Zitto Kabwe, aliomba Muongozo ili Bunge lijadili hatua ya TBC1 kutoonesha Bunge live wakati inapewa ruzuku na Serikali.

Mara ya Kwanza Chenge alikataa kumpa nafasi Zitto ya kuongea, lakini baada ya Kambi ya upinzani kuanza kupiga kelele, akaamua kustisha bunge kwa saa moja ili kamati ya Uongozi ikae kujadili hilo swala.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname