Siku chache baada ya mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa
kupinga matokeo rasmi yaliyotolewa na NEC yakimtangaza Dkt. John
Magufuli kuwa mshindi na Rais Mteule anayesubiriwa kuapishwa, viongozi
wa Ukawa wameelekea Ughaibuni kutafuta msaada wa kisheria.
Taarifa
kutoka kwa chanzo cha kuaminika zimeeleza kuwa, viongozi hao wameelekea
Uholanzi kutafuta msaada ya kisheria ili kufahamu hatma yao kwani
wanaamini mgombea wao alishinda nafasi ya urais kwa asilimia 62, takwimu
zilizotofautiana na matokeo yaliyotangazwa na NEC yakionesha alipata
asilimia 39.97.
“Viongozi wetu wapo Uholanzi kwenye mazungumzo nyeti juu ya kilichotokea, soon watatupa mrejesho. Letz stay calm.!”
Taarifa
hizo ziliambatana na picha inayomuonesha mwenyekiti wa Chadema, Freeman
Mbowe akiwa na mwanasheria wa Chama hicho wakiongea na ‘wazungu’ katika
eneo lilitajwa na chanzo hicho kuwa ni Uholanzi.
Hata hivyo, katiba ya nchi hairuhusu matokeo ya urais yaliyotangazwa na NEC kuhojiwa mahakamani.
Wakati
Tume ya Uchaguzi ikimtangaza Dkt. John Magufuli wa CCM kuwa mshindi wa
nafasi ya urais kwa asilimia 58.46, Mgombea urais wa Chadema Edward
Lowassa alidai kuwa takwimu walizonazo kutoka vituoni zinaonesha kuwa
yeye ndiye mshindi na alipata asilimia 62 ya kura zote.

No comments:
Post a Comment