22 June 2015

Kauli ya Mzee Majuto kuhusu Wema Sepetu kuwania Ubunge

Wiki iliyopita Wema Sepetu alitangaza nia yake ya Kugombea Ubunge huku mastaa Mbalimbali wakijitokeza kumpa hongera kwa uamuzi wake huu wa kugombea ubunge wa viti maalumu.4f9511352282_1608022146123896_1362237940_n

Mmoja kati ya wasanii waliojitokeza kumuunga mkono Wema Sepetu ni Mwigizaji Mzee King Majuto.
Mzee Majuto kapost katika mtandao wa Instagram na Kuandika haya:

“Nisingependa kuyaongea haya kwenye mfungu mtukufu ila kiundani ningependa kuonyesha umoja na kumuunga mkono wazo na lengo la Mwanangu kwa kuwa anaweza na amethubutu sasa isitokee wale wasiopenda maendeleo ya watu na taifa hili kuvuruga misingi na mipango madhubuti ya kuwapa nafasi vijana na hasa wanawake kushika hatamu na kuleta mabadiliko.Kapeleke mabadiliko Singida na Tanzania nzima. Muhimu ni kuwa na juhudi uwezo imani pamoja na uzalendo. Ujumbe huu pia ni kwa kila kijana na mwanamke mwenye lengo na nia ya udhubutu. Inshallah. Ramadhan Maqbul Waislam wote.”

- See more at: http://patahabari.com/2015/06/21/kauli-ya-mzee-majuto-kuhusu-wema-sepetu-kuwania-ubunge/#sthash.x1xzxGWv.dpuf

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname