24 June 2015

HIVI NDIVYO ALI KIBA ALIVYO PANDA DALADALA NA KUKOSA SITI NA KUAMUA KUSIMAMA JIJINI DAR LEO HII



Mshindi wa tuzo tano za KTMA 2015, Alikiba amewapa mashabiki wake nafasi ya kuonana naye baada ya kuamua kutumia usafiri wa daladala kuzunguka jijini la Dar es Salaam.Muimbaji huyo wa Chekecha alianza safari yake kwa kupanda daladala ya Kariakoo/Mbagala na kutangaza kwa abiria nia yake ya kupanda daladala nao ikiwa ni pamoja na kuwalipia nauli.
Akizungumza na mashabiki kwenye daladala hizo, Alikiba alisema ameamua kupanda daladala kwa kuamini ataweza kukutana na mashabiki wake ambao hawawezi kumuona na kumpa dukuduku zao juu ya muziki anaofanya.“Nimepanda ndani ya daladala pamoja nanyi kutokana na mapenzi mnayonionyesha katika kazi zangu,” Alikiba aliwaambia abiria wa daladala aliyokuwa amepanda. 

“Nisingeweza kuwakusanya pamoja watu wote ila nimeona kwa njia hii ninaweza kuonana na baadhi ya mashabiki wa muziki wangu ambao hawana uwezo wa kuonana na mimi. Lakini kubwa zaidi ni kuwashukuru na kunichagua kuwa msanii ninayependwa. Nimepewa tuzo nyingi kwaajili yenu sina cha kuwalipa zaidi ya shukrani tu. Pia kila mmoja ndani ya daladala nimemlipia nauli, kwahiyo kama kuna yoyote mwenye maoni au ushauri au swala anaweza uliza,” aliongeza staa huyo.
Baada ya kauli hiyo mashabiki mbalimbali walitoa shukrani zao, huku shabiki mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Ashura Khamis akimtaka Alikiba kuzungumzia ugomvi wake na Diamond pamoja na uwezekano wa kufanya kolabo.“Sina ugomvi na mtu yoyote, mambo ya kolabo yanawezekana ila ni masuala kiuongozi zaidi,” alijibu Kiba na shabiki huyo kuonekana kuridhika na jibu.


Ali Kiba akishuka kwenye basi la Mbagala, Kariakoo Alikiba akishuka kwenye basi la Mbagala

Ali Kiba akiwa ndani ya basi la abiria Alikiba akiwa ndani ya basi la abiria

Ali Kiba akipiga stori na abiria Alikiba akipiga story na abiria

Ali Kiba akishuka katika kituo cha Mtongani Alikiba akishuka katika kituo cha Mtongani
Ali Kiba akishuka kwenye daladala ya Tememe Alikiba akishuka kwenye daladala ya Temeke

Ali Kiba akiwa katika kituo cha basi Msimbazi Center Alikiba akiwa katika kituo cha basi cha Msimbazi Center

Ali Kiba akiwa pamoja na abiria ndani ya daladala ya Temeke/Kariakoo Alikiba akiwa pamoja na abiria ndani ya daladala ya Temeke/Kariakoo
IMG_1063
IMG_1064
IMG_1070
IMG_1072
IMG_1074
IMG_1075
IMG_1081
IMG_1085
IMG_1096
IMG_1099
IMG_1100
IMG_1107

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname