Kwa mujibu wa ‘shujaa’ wetu, tukio hilo la aibu ya aina yake lilijiri juzikati kwenye Ukumbi wa Savoy mjini hapa ambapo wanawake hao walialikwa kuburudisha kwenye sherehe ya harusi ya jirani yao. Mtu mzima ovyoo! Akina mama watatu ambao ni wake za watu, wanaounda Kundi la Heshima Pesa Shikamoo Makelele lenye maskani yake maeneo ya Mawenzi mjini hapa wanadaiwa kuwachefua baadhi ya watu baada ya kujitoa fahamu na kumwaga ‘lazi’ hadharani na mbaya zaidi mbele ya watoto wadogo.
Wanawake hao waliofahamika kwa majina ya watoto wao ni pamoja na mama Sabra aliyekuwa akibinuka, aliyevalia kigauni kifupi cha draftidrafti.Mwingine alikuwa ni mama Jenifa aliyekuwa ametupia kimini cha njano na mama Athuman ambao kwa pamoja walikuwa na vikuku miguuni.
Mtu wetu huyo aliyekuwa ndani ya ukumbi huo aliwashuhudia wanawake hao wakimwaga lazi mara baada ya MC kuita kundi lao kwa ajili ya kutoa zawadi.
No comments:
Post a Comment