Hapa
nyumbani Tanzania nimeshawahi kusikia kuhusu matajiri wachache
wanaofanya biashara ambao huwa hawabadili nguo zao au huwa kuna vitu
wanafanya vinavyopelekea hisia za watu kuamini kwamba utajiri wao ni wa
uchawi.
Mfano
kuvaa nguo ya aina moja hiyohiyo kila wakati, wengine huwa wanatembelea
magari mabovu kabisa lakini watoto wao na wake zao wanatembelea magari
makali na wanabadilisha kila wakati, wengine tunaambiwa wanalala
barazani.
Sasa
hii ya tajiri wa mtandao wa kijamii wa Facebook wenye watumiaji zaidi
ya bilioni moja kote duniani Mark Zuckerbeg sijui watu wataiweka kwenye
kipande gani manake ameonekana mara nyingi sehemu na nyakati tofauti
akiwa amevaa Tshirt moja tu ya kijivu.

Ni
swali ambalo Waandishi wengi waliwahi kutamani kupata time ya kumuuliza
ambapo kwa bahati nzuri kaulizwa kwenye kipindi cha maswali na majibu
na akatoa jibu akiwa na tabasamu zito kabisa.
‘Nimepata
hii bahati ya kipekee kuwa kwenye nafasi niliyonayo, ninaamka kila siku
na kuwahudumia zaidi ya watu bilioni moja duniani… naona sitofanya kazi
yangu vizuri kama nitatumia muda wangu kwenda kutafuta/kuchagua nguo
nzuri, tshirt mnayoniona nayo ni ya rangi moja lakini nilizinunua nyingi
za namna hii’
‘Ni
Tshirt ambayo sio moja… ninazo nyingi ila zinafanana, muda wangu mwingi
nimeutenga kwa ajili ya kuhudumia watu na sio kujihudumia mimi kwenye
kuchagua nguo nzuri, mavazi ni kitu kidogo sana kwangu’
No comments:
Post a Comment