Louis van Gaal na Truus wamejiunga na Manchester United kuanza ukurasa mpya wa maisha ya mpira.
LOUIS
van Gaal haogopi kukosolewa na mashabiki pamoja na vyombo vya habari,
anasema mtu anayemfahamu vizuri mno kocha huyo mpya wa Manchester
United.
Mke
wake Van Gaal, Truus van Gaal, ameweka wazi kuwa kocha huyo wa zamani
wa Ajax, Barcelona na Bayern Munich, hawezi, hajawahi kukata tamaa pale
anapokosolewa isipokuwa anaumia sana anaposhindwa kufanya kazi yake
vizuri au anapomuumiza yeye.
Watu wote wa Old Trafford watakuwa na
furaha kusikia kuwa inachukua muda mrefu kumuudhi kocha huyo mwenye
miaka 62-isipokuwa mke wake anayechukizwa na watu wanamuudhi mume wake.
Truus alisema:
Louis haogopi kukosolewa Hata kama timu yake imecheza vizuri au vibaya,
hata kama watu au vyombo vya habari vitamponda au hapana, haathiriwi na
kitu chochote. Mara zote ananiambia Unaogopa nini? waache wafurahie
haki yao. Wewe tu ndio nakuogopa na najua mambo yalivyo kiuhalisia.
Kitu pekee kinachomuudhi ni kuona mimi naumia au nakata tamaa
Truus alikiri kuwa hafanani na mume wake kwasababu yeye anaguswa sana na matusi.
Siku za nyuma, nilienda kwenye mechi ya mpira wa miguu na kulikuwa na
mtu mbele yangu akamtukana Van Gaal Nilimshika mabegani na kumkalipia
Amekufanyia nini unamjua? mtu huyo aliogopa sana. Kocha mpya wa
Manchester United, Van Gaal, falsafa yake ni kucheza mpira wa
kushambulia.


No comments:
Post a Comment