Kampuni ya pili kwa ukubwa katika
utengenezaji wa sigara nchini Marekani imeagizwa kulipa kitita kikubwa
cha dola billioni 23 kwa mke wa mwathiriwa mmoja wa sigara aliyefariki
kutokana na saratani ya mapafu.
Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC,
Mjane huyo Cynthia Robinson alichukua hatua dhidi ya kampuni ya sigara
ya R.J Reynolds baada ya kifo cha mumewe aliyekuwa na miaka 36.
Kampuni hiyo imeyataja malipo hayo kama yasio na haki na kusema kuwa itakata rufaa.
Wakili wa bi Robinson amesema kuwa kampuni hiyo ya sigara iliuza sigara
hizo bila kutoa tahadhari yoyote kuhusu tishio la uvutaji wake.

No comments:
Post a Comment