16 April 2014

TIZAMA HAPA JINSI LOWASSA ALIVYOMKARIBISHA RAIS MSTAAFU MKAPA WILAYANI MONDULI

Rais mstaafu wa awamu wa tatu Mh Benjamin Mkapa amefanya ziara kutembelea shule ya msingi ya Manyara Ranchi inayofadhiliwa na shirika la kimataifa la uhifadhi wa wanyamapori la African Wildlife Foundation  Wilayani Monduli. Mzee Mkapa ni Makamu Mwenyekiti wa shirika hilo lenye makao yake mjini Washington Marekani. picha mbalimbali zinamuonesha Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akimuongoza Rais Mkapa kuzuru shule hiyo.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akizungumza Mzee Mkapa Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akiagana na  Mzee Mkapa
 
NA: RWEYEMAMU BLOG

2 comments:

  1. imependeza sana. Tudumishe upendo watanzania ndo chachu ya mafanikio

    ReplyDelete
  2. Tanzania tumetoka mbali sana jamani mpaka sasa tulipo inabidi tujipongeze kwa amani tuliyokuwanayo.
    Tuipongeze selikari yetu iliyo madarakani kwa makubwa iliyo fanya, tuachane na viongozi wagombanishi na wasiopenda amani iendelee.
    Tujenge nchi yetu kwa selikari imara na wananchi waliojaa upendo na ukarimu.
    Amani ndio jambo la msingi hasa kwa mtu yeyote yule anayependa maendeleo katika shughuli zake. Namalizia kwa kusema selikari mbili ndio mhimili mkubwa na wenye kupunguza gharama kwa watanzania tuachane na viongozi wanaopenda maslahi yao.
    Amani idumu kwa kula mtanzania

    ReplyDelete

Comments system

Disqus Shortname