10 March 2014

MSIKILIZE JAMAA AKIZUNGUMZA BAADA YA DAWA ZA MARALIA KUMBADILISHA NA KUWA ALBINO.

Pichani: Hafidhi kabla na baada ya kutumia Metakelfin
Hafidh Masokola mwenye umri wa miaka 47,  mkaazi wa Tabora amedai kuwa alitumia dawa aina ya Metakelfin miaka minne iliyopita kwa lengo la kutibu ugonjwa wa malaria, lakini dawa hizo zilimsababishia madhara makubwa katika ngozi yake na kumpelekea kuwa albino.
Akiongea na Sun Rise ya 100.5 Times Fm, Hafidh ambaye ni mjasiriamali ameeleza kuwa alinunua dawa hizo ‘Pharmacy’ na kwamba baada ya kumsababishia madhara hayo ameamua kujiunga na chama cha maalbino Tanzania kwa kuwa anafanana na albino wengine.
BOFYA HAPA KUSIKILIZA

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname