10 December 2013

HUU UGOMVI NA PREZZO NA HUDDAH UNAPOELEAKEA....!! AU NDIYO KUSAKA UMAARUFU...??

Huddah Monroe Uhasama mkali unaozidi kuchemka kati ya rapa mbishi CMB Prezzo na 'msocialite’ Huddah Monroe wameamua kuanikana wazi na kuzitoa siri zao za ndani kwenye mtandao.


Tatizo nzima lilianza pale Huddah alipomkashifu Prezzo kwenye akaunti yake ya Instagram akimtaja kuwa mtu aliyeishiwa na anayependa kudekezwa sana.
Kama kawaida yake 'king wa maBling’ alijibu mpigo kwa kumwita Huddah kiruka njia asiyejielewa na ambaye yupo tayari kutumiwa na kila mtu.
Kipusa huyo naye hakuchoka kumjibu akisema kwamba kheri kuwa kiruka njia kuliko kuwa mtu wa kutegemea mamake hata katika umri mkubwa kama wake Prezzo
Majibizano yalizidi kuwa makali huku wawili hao wakitupiana cheche zaidi yenye soni kwenye akaunti zao mbalimbali za mtandaoni ikiwemo Twitter.

Letu ni jicho tu maana hatujui picha hii mbaya kati ya wawili hawa itaishia wapi, au labda ndio suala nzima la kusaka umaarufu.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname