11 November 2013

HII NDO SABUNI YA KUOGEA YENYE BEI KULIKO ZOTE INAUZWA TSH.MILIONI 6



Kuoga kifahari kumepata maana mpya baada ya Qatar kuzindua sabuni ya kuogea yenye gharama kubwa zaidi duniani iliyotengenezwa kwa vumbi la dhahabu halisi, mafuta ya olive na asali huku ikiwa imebadikwa madini ya almasi.

Kipande hicho cha sabuni kina uzito wa 100gm na kina thamani ya dola $3,800 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 6.

Sabuni hiyo iitwayo . ‘Qatar Royal Soap’ imetengenezwa kuonesha mafanikio ya Qatar ikiwemo kushinda nafasi ya kuandaa kombe la dunia FIFA 2022.

Hata hivyo sabuni hiyo iliyotengenezwa na Khan Al-Saboun Bader Hassoun and Sons, haitakuwa ya biashara.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname