Mkurugenzi wa brand ya urembo ya Kidoti, Jokate Mwegelo akifurahia jambo na mama yake mzazi, Benadertha Ndunguru.
Akizungumza
mara baada ya mwanaye kusaini mkataba huo kwenye Hoteli ya Serena,
Dar, mwishoni mwa wiki iliyopita, mzazi huyo alimmwagia Jokate sifa tele
na namna anavyofurahishwa na maendeleo yake.Vunja ukimya! Kwa mara ya
kwanza, mama mzazi wa mwanamitindo na mkurugenzi wa brand ya urembo ya
Kidoti, Jokate Mwegelo, Benadertha Ndunguru amemfungukia mwanaye baada
ya kuingia ubia na Kampuni ya Rainbow Shell Craft ya nchini China
inayomuingizia mabilioni ya fedha.
Jokate Mwegelo akilamba dili nono kutoka kwa wachina.
“Jokate
ni mwanangu wa tatu kuzaliwa. Najivunia akili yake, uwezo wake, namna
anavyojituma, namshukuru sana Mungu kwani anafanya mambo makubwa
kulingana na nafasi yake,” alisema mama Jokate.
Jokate Mwegelo akipiga picha na mwakilishi wa kampuni ya Rainbow Shell Craft ya nchini China.
Kwa
upande wake, Jokate aliliambia Ijumaa Wikienda kwamba amefurahishwa na
ubia huo kwani mbali na masuala ya urembo pia kupitia brand yake
anatarajia kuongeza ajira kwa akina mama kwani kitajengwa kiwanda
ambacho kitatoa ajira kwao.
Jokate Mwegelo na mama yake mzazi wakipata picha ya ukumbusho na wadau wengine.
“Hii
ni fursa kubwa kwetu Tanzania, nawashukuru sana vijana wenzangu ambao
tulikaa na kubuni brand ya Kidoti, leo imenipa heshima kwa Watanzania na
inakuja kutufaidisha,” alisema Jokate.
No comments:
Post a Comment