11 November 2013

KIGOGO CCM ATOLEWA UTUMBO...KISA CHASHANGAZA.

Mwenyekiti wa CCM Kijiji cha Chole wilayani Kisarawe, Pwani, Kondo Shamte baada ya kuchomwa mkuki tumboni na wafugaji wa kabila la Wamang’ati.

MWENYEKITI wa CCM Kijiji cha Chole wilayani Kisarawe, Pwani, Kondo Shamte (36) yuko katika hali mbaya baada ya kuchomwa mkuki tumboni na wafugaji wa kabila la Wamang’ati na kusababisha utumbo wake kuwa nje, paparazi limeinasa hiyo.
Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo ambaye kwa nafasi yake kijijini hapo ndiye anayeheshimika zaidi, tukio hilo lilijiri Agosti 28, mwaka huu.Akizungumza kwa masikitiko makubwa nyumbani kwake kijijini hapo, Kondo alisema katika kijiji hicho kulijengwa barabara na wahisani (hakuwataja jina). Wanakijiji wakaombwa kuitunza barabara hiyo kwa masharti kwamba wasipitishe mifugo.

 

Utumbo wa Kondo Shamte ukiwa nje baada ya kuchomwa mkuki.
Alisema siku ya tukio, wafugaji hao walipitisha mifugo katika barabara hiyo licha ya amri iliyokuwepo, alipoona hali hiyo aliwafuata na kuwaomba wapitishe pembeni.
“Walikataa, nikaamua kuwatuma wajumbe wangu wawafuatilie kwa nyuma ili wasiendelee kupitisha mifugo hiyo,” alisema mwenyekiti huyo.
 

Kondo Shamte akiuguza jeraha lake tumboni.
Akaendelea: “Baada ya wafugaji hao kuona nimetuma wajumbe wakarudi hadi nilipokuwa nimesimama na kuniambia kuwa niliwatuma wale wajumbe ili wakawafanyie fujo, wakatoa vitisho kwamba ule ndiyo ungekuwa mwisho wangu.

Mwenyekiti huyo aliendelea kusema kuwa kabla yeye hajazungumza chochote, mfugaji mmoja alichomoa mshale na kumrushia ambapo ulimwingia tumboni kisha wote wakakimbia.

Alisema alijitahidi sana kuutoa mshale huo huku tayari akiwa ameanguka chini. Alipofanikiwa, ndugu na jamaa nao walitokea na kumkimbiza Hospitali ya Kisarawe.

“Pale hospitalini Kisarawe ilishindikana kunitibu, nikakimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Dar es Salaam) ambako nilifanyiwa upasuaji mkubwa kwa kukata  sehemu ya utumbo iliyoharibika,” alisema.

Mwenyekiti huyo aliendelea kuweka wazi kwamba baada ya operesheni hiyo daktari alimwambia ni lazima sehemu ya utumbo utolewe nje mpaka sehemu ya ndani ipone vizuri ndipo waurudishe, hivyo kwa sasa haja kubwa anaitolea ubavuni.

“Hivi sasa haja kubwa natolewa kwa hapa ubavuni mpaka nitakaporudi tena hospitali mwezi Desemba, mwaka huu,” alisema.

Hata hivyo, Kondo alisema kitu kinachomuuma zaidi na kutomuona kiongozi wa CCM hata mmoja aliyefika nyumbani kwake kumjulia hali wala kumpa msaada wowote kwani hivi sasa yuko katika hali ngumu ya kimaisha kutokana na gharama za kutibu kidonda chake kuwa juu

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname