27 October 2013

WASTARA HAFIKIRII KUOLEWA KWA SASA, SAJUKI BADO YUPO MOYONI MWAKE.


 

Kufuatia habari iliyotoka juzi baada ya kuandikwa na gazeti moja la udaku na baadaye kusambaa mitandaoni kuwa muigizaji maarufu nchini Wastara Juma Sajuki anafikiria kuolewa ikiwa ni takribani mwaka na miezi kadhaa tangu aliyekuwa mume wake na star wa filamu pia Juma Kilowoko(Sajuki) kufariki dunia, muigizaji huyo amefunguka ya moyoni mwake kupitia page yake ya facebook akionekana hana mpango wa kuolewa leo au kesho bali Sajuki bado yupo moyoni mwake. Star huyo wa filamu za Vivian, Mboni Yangu, Kivuli na Vita aliandika hivi jana katika page yake "Milele uko ndani ya moyo.wangu kokote niendako nipo nawe ni kazi sana kuziba pengo langu, nakupenda ni wewe tu Haupo kimwili lakini umeondoka na umeondoka na nusu ya akili yangu huku hakuna linalofanyika bila kuvuta taswira yako nakupenda sana Sajuki"

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname