10 June 2014

Rihanna Awajibu TLC Waliomponda Kuwa Anauza Ngono kwa Kuvaa Nusu Mtupu


Vazi la Rihanna katika tuzo za mitindo za CFDA mwaka huu limeendelea kuwa gumzo na wengi wamemshambulia kwa madai ya kutojali maadili.
Member wa kundi la TLC, Chilli na T-Boz nao hawakusita kumpa makavu live wakati wanafanya mahojiano na kipindi cha SunRise cha televisheni ya Australia. Walisema kuhusu mavazi hayo na kueleza kuwa Rihanna anauza ng9no.


“Ni vigumu kwetu kusema kitu kwa sababu wakati wowote tukifanya hivyo, ‘oh, lazima TLC wanaona wivu’, lakini hivyo ndivyo ilivyo. Naliita koleo..koleo.

“Sisi tuliuza na kuwa kundi kubwa la wasichana la muda wote lililouza zaidi, tukiwa tumevaa nguo zetu. Ni rahisi kuuza ng9no.” Amesema T-Boz.

Ujumbe umemfikia Rihanna nae hakulaza damu akajibu mashambulizi. Kwanza alibadili picha yake ya Twitter (Twitter header) na kuweka picha ya wasichana hao wa TLC, Chilli na T-Boz wakiwa vifua wazi. Katika picha hiyo wasichana hao wawili wanaonekana wakiwa wamefunika vifua vyao na mikono.

Baadae alibadili na kuweka picha yake akiwafanya mzaha na kutoa ulimi nje, halafu akaiandika,

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname