Wananchi 6,700 wa Kata ya Kilolambwani wilayani hapa wanakabiliwa na tatizo kubwa la upungufu wa chakula na kusababisha baadhi ya wananchi kula mizizi ya porini.
Hayo yamebainishwa na Diwani wa Kata hiyo, Salamu
Matajabu pamoja na wenyeviti wa Serikali za Vijiji vya Nangole na Dimba
wakati walipokuwa wanazungumza na timu ya waandishi wa habari kwa
nyakati tofauti mjini Lindi jana.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Dimba,
Abdalla Mbwana amesema hali ya chakula kwa wananchi wake ni mbaya jambo
linaloweza kusababisha baadhi ya wakazi wa kijiji hicho kupoteza maisha
kutokana na kukosa chakula.
Naye Diwani wa kata ya Kilolambwani Salamu Mtajabu
alisema tatizo la njaa katika eneo hilo limevikumba vijiji saba
vinavyounda kata hiyo lililosababishwa na ukosefu wa mvua kwa misimu
miwili mfululizo wa 2010/11 na 2012/13.
Matajabu alisema zinahitajika juhudi za makusudi
na haraka kuwapatia msaada wa chakula wananchi hao ili kuokoa maisha ya
wakazi hao .
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Dk Nasoro
Himidi alisema tatizo la upungufu wa chakula katika kata hiyo, ofisi
yake inalitambua na tayari ameomba tani 19,000 za nafaka Ofisi ya Waziri
Mkuu, Kitengo cha Maafa .
Hata hivyo katika utafiti wa hivi karibuni
imebainika kuwa takribani wa watu Milioni 840 wanakabiliwa na upungufu
wa chakula duniani,huku watu bilioni 2 wakikabiliwa na tatizo la lishe
na chakula bora wakati bilioni 7 wakiwa katika hatari ya kushambuliwa na
utapia mlo duniani Afrika ikiongoza.
Sorce: Mwananchi
Sorce: Mwananchi
No comments:
Post a Comment