Wakizungumza kijijini hapo wananchi hao wamesema wameamua
kuandamana na kufunga barabara kufuataia shirika la umeme Tanesco
kushindwa kusambaza huduma hiyo katika kijiji hicho na badala yake
kupitisha nguzo katika maeneo yao kupeleka huduma katika vijiji vya
jirani ambapo wamesema hawapotayari kuruhusu mradi huo kuendelea hadi
watakapohakikishiwa kuunganishiwa nishati hiyo.
Nao viongogozi wa kata na kijiji cha Lumuma wamesema wanaunga mkono
wananchi kwani wamesema inaonekana zoezi hilo limegubikwa na hujuma
huku wameomba serikali na uongozi wa Tanesco kuona uwezekano wa kuanza
kusambaza umeme katika kijiji cha Lumuma na badaye kumalizia katika
vijiji vilivyoko katika kata hiyo.
Akiongea na ITV kwa njia ya simu meneja Tanesco mkoa wa Morogpro
Mhandisi John Bandiye amesema anatambua kuwepo mradi wa umeme katika
kata ya Lumemo lakini hafahamu kama wananchi wa kijiji hicho
wanalalamika na kwamba atafuatilia ili kulitafutia ufumbuzi tatizo
hilo.
No comments:
Post a Comment