
Goldie na Prezzo.
Taarifa ambayo kila aliekua
karibu na Goldie kwenye page zake za facebook na twitter inakua ngumu
kuamini, taarifa rasmi zimeripoti kwamba Goldie ambae ni mwakilishi wa
Nigeria kwenye BBA 2012 AMEFARIKI muda mfupi tu baada ya kuwasili Lagos
Nigeria akitokea Marekani ambapo bado chanzo cha kifo chake
hakijajulikana.
Mmoja wa wasaidizi wake
amethibitisha kifo cha Goldie kupitia page ya twitter ya Goldi kwa
kusema ni kweli msanii huyo amefariki dunia usiku wa february 14 2013
muda mfupi tu baada ya kuwasili Lagos Nigeria, hali yake ya afya
ilibadilika ghafla ikabidi apelekwe
hospitali ambako hakuchukua muda
mrefu akafariki dunia.
Taarifa nyingine nilizozipata
kutoka kwa mtu wake wa karibu wanaeshirikiana kimuziki zimeeleza kwamba
mpenzi wake Goldie ambae ni Msanii wa Kenya CMB Prezzo ametua Nigeria
usiku huu muda mfupi uliopita kwa ajili ya kuendeleza mipango aliyokua
nayo na Goldie ikiwemo kutengeneza show ya TV.
Prezzo alitakiwa kushiriki
katika TV show ambayo yeye na Goldie wangekua moja ya wahusika wakuu
ambapo mpango ulikua baada ya mwezi mmoja Goldie na Prezzo wangekuja
Tanzania, Uganda na Kenya kwa ajili ya kujitangaza na kuipromote single
mpya ya Goldie ya ‘Skibobo’ aliyofanya na Ay.

.

Huyu
Deji ni mtangazaji wa Radio huko Nigeria ambae Goldie ndio
aliniunganisha nae, muda mfupi baada ya kupata taarifa za Goldie ilibini
nimtumie msg ili kujua kama ni kweli, na majibu yake ndio hayo hapo
juu.
Kwenye Exclusive interview na millardayo.com october
19 2012 alisema alikua na mpango wa kwenda Marekani kurekodi kolabo
yake na mastaa wawili wa muziki ambao ni Keri Hilson na Trey Songs ambao
tayari mipango ilikua tayari na kilichobaki ilikua ni makubaliano ya
mwisho mwisho tu.

Marehemu Goldie kwenye interview na Millard Ayo wakati alipokuja Tanzania kurekodi single yake ya ‘Skibobo’ na Ay.

Hizi ni tweet na picha alizopost akiwa Marekani juzi.

.
source millrad ayo